Combination mpya 65 za form five 2024 – Jinsi ya Kubadilisha Combination

0

Combination mpya 65 za form five 2024 –  Selform Tamisemi go tz 2024

Combination mpya 65 za form five 2024

Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI imekamilisha zoezi la awali la kuingiza kwenye kanzidata taarifa zilizo kwenye Fomu za Uchaguzi za wanafunzi kama zilivyojazwa na wanafunzi wakiwa shuleni. Aidha, napenda mtambue kuwa Mabadiliko ya Sera ya

Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023 na Mitaala ya Elimu kwa Kidato cha Tano yameanza kutekelezwa, ambapo utekelezaji huo umehusisha uanzishaji wa Tahasusi mpya 49, kutoka 16 zilizokuwepo awali hadi kufikia tahasusi 65. Tahasusi hizo mpya zitakazoanza kutekelezwa Julai, 2024 zipo katika makundi saba (7) ambayo ni: Tahasusi za Sayansi ya Jamii; Tahasusi za Lugha; Tahasusi za Masomo ya Biashara; Tahasusi za Sayansi; Tahasusi za Michezo; Tahasusi za Sanaa; na Tahasusi za Elimu ya Dini. Orodha ya masomo na Tahasusi zitakazoanza kutekelezwa Julai, 2024.

Kukamilika kwa zoezi hili kunatoa fursa kwa wanafunzi kuweza kufanya mabadiliko ya machaguo/ tahasusi/ kozi kwa njia ya
mtandao (online). Baada ya wanafunzi kufanya marekebisho yao, kanzidata hiyo ndiyo itakayotumika kuwachagua na kuwapangia nafasi za Kidato cha Tano na Kozi mbalimbali katika Vyuo vya Kati na vya Elimu ya Ufundi kwa kuzingatia sifa za ufaulu na machaguo yao.

Ofisi ya Rais – TAMISEMI inatoa fursa kwa wahitimu wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Nne mwaka 2023 kubadili machaguo yao ili kutoa nafasi zaidi kwa Mwanafunzi kusoma tahasusi au kozi itakayomwandaa kuwa na utaalam stahiki katika maisha yake ya baadaye. Hii ni kutokana na ukweli kwamba wakati wa ujazaji wa fomu za machaguo ya awali, tahasusi mpya 49 hazikuwepo kwenye orodha ya machaguo na pia matokeo ya mtihani wa kuhitimu Kidato cha Nne hayakuwa yametoka kumuwezesha mwanafunzi kuweza kuwa na machaguo mazuri zaidi kulingana na ufaulu wake. Hivyo,
zoezi hili litatoa fursa zaidi ya wanafunzi kuongeza machaguo na kufanya machaguo mapya ya Tahasusi na Kozi. Napenda kuwasihi wazazi/walezi kushiriki katika zoezi hili kwa kushauriana na watoto wao katika kufanya machaguo sahihi kulingana na ufaulu wao.

Jinsi ya Kubadilisha Combination/Tahasusi

Kwa umuhimu huo, wahitimu wote wanahimizwa kufanya marekebisho ya machaguo ya tahasusi na kozi kulingana na ufaulu wao, kwa kuingia kwenye Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi (Student Selection MIS) unaopatikana kupitia kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz. Aidha, maelekezo kwa wahitimu na jinsi ya kufanya mabadiliko yanapatikana kwenye mfumo wa uchaguzi wa wanafunzi. Ili kuingia kwenye mfumo itabidi mhitimu atumie Namba ya Mtihani wa kuhitimu Kidato cha Nne mwaka 2023, Jina lake la Mwisho, Mwaka wa Kuzaliwa na Alama ya Ufaulu aliyopata kwenye somo atakaloulizwa na mfumo au swali lolote atakaloulizwa.

Zoezi la kubadilisha tahasusi na vyuo litaanza rasmi tarehe 20 Machi, 2024 hadi tarehe 30 Machi, 2024. Wanafunzi, wazazi na walezi wanakumbushwa kushauriana kikamilifu ikiwa ni pamoja na kupata ushauri wa kitaalam na kitaaluma kabla ya kufanya mabadiliko ya tahasusi au Kozi.

Ninawasisitiza wanafunzi, wazazi/ walezi kutumia muda huo vyema ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza mara baada ya matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo kutangazwa. Ni muhimu kuzingatia muda uliotolewa wa kufanya marekebisho ili ratiba ya kuwachagua na kuwapangia shule na vyuo iweze kuendelea kwa muda uliopangwa. Baada ya matokeo ya kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo kutangazwa, Ofisi haitashughulikia changamoto hizo kwa kuwa fursa ya kufanya mabadiliko hayo imeshatolewa.

Leave A Reply

Your email address will not be published.