TAMISEMI Yasema inaajiri Walimu 11000 mwezi ujao

TAMISEMI Yasema inaajiri Walimu 11000 mwezi ujao
0

TAMISEMI Yasema inaajiri Walimu 11000 mwezi ujao

TAMISEMI ajira za walimu 2024: Wakati wadau wa elimu wakihoji utayari wa serikali kuwahudumia wanafunzi wataakaochagua tahasusi 65, waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, amesema wamejipanga kibajeti, walimu na miundombinu.

amesema watanzania hawapaswi kuwa na hofu juu ya utekelezaji wake, kwani maandalizi yamaekwishafanyika na walimu 11,000 wapya wataajiriwa. Alitoa maelezo hayo siku moja tangu alipotangaza tahasusi mpya 49 za masomo mbalimbai  ambapo awali kulikuwa na tahasusi 16 pekee.

Tahasusi izo zimetengwa kwenye makundi saba na zitaanza kutumika Julai mwaka huu. Makundi hayo ni Sayansi ya jamii, Lugha, maomo ya biashara, tahasusi za sayansi, michezo, sanaa na elimu ya dini. Juzi Mchengerwa alitanja sababu ya kuanzishwa kwa tahasusi hizo, kuwa ni utekelezaji wa mabadiliko ya sera ya elimu ya mafunzo ya mwaka 2024 toleo la 2023 na mitaala ya elimu ya kidato cha tano.

Mara baada ya kuzitangaza tahasusi izo, kuliibuka mijadala mbalimbali kutoka kwa wadau, wapo waliopongeza wakisema zinafungua fursa kwa wanafunzi kuwa na mwanda wa kuchagua tahasusi na wengine wakihoji utayari wa serikali.

Maandalizi ya utekelezaji wa Tahasusi izo

Katika hoja hizo za wadau, Waziri mchengerwa kwenye mahojiano muhimu jana, alisema Watanzania hawapaswi kuwa na hofu juu ya utekelezaji wa tahasusi izo akisema: “katika hili serikali imejipanga vizuri na wala haijakurupuka”. Waziri mchengerwa aliongeza kwa kusema kuwa “Sisi TAMISEMI kwa ushirikiano na wizara ya elimu tumeshajipanga vizuri kuhakikisha tunao wataalamu wa kutosha kuhakikisha taunatibu tatizo ilo.”

Miongoni mwa mkakati aliyotaja ni kuajiri walimu 11,000 ifikapo Aprili mwaka huu watakaokwenda kupunguza upungufu wa walimu. “Mheshimiwa Rais ameshatoa vibali vya ajira takribani walimu 11,000 tunaokwenda kuajiri kuanzia mwezi unaokuja, watakaokwenda kufiti kwenye maeneo ambayo kuna uhaba wa walimu katika baadhi ya tahasusi nilizozungumza hapo awali,” alisema Mchengerwa.

Kuhusu Bejeti, waziri Mchengerwa alisema serikali tayari imejipanga na imefanya mazungumzo na Benki ya Dunia (WB) walioahidi kusaidia. “sasa huwezi kusaidiwa kama hujaonesha eneo unalotaka kusaidiwa na katika hili kama mnavojua tumeanzisha madarasa mtandao” alisema.

Waziri Mchengerwa alitaja matumizi ya Teknolojia ya digitali katika kufundisha ili kukabiliana na upungufu wa walimum akisema mwalimu mmoja anweza kufunsisha nchi nzima tukiwa tumefunga madarasa mtandao. ” Mwalimu mmoja anaweza kufundisha shule 100,200 au hata 500. Eneo hili tumeshaweka mikakati kwa kuwataka wakurugenzi wa halamshauri katika maeneo ya kuweka bejeti. “Moja ya mkakati ni kuhakikisha kunakuwa na vifaa vya kidigitali katika shule zetu na tumeshauri kila halmashauri ihakikishe imekuwa na shule moja kwakuanzia, ambapo mwalimu anaweza kukaa pale kibaha (Mkoa wa Pwani) au akakaa Dodoma shule zote nchini akazifundisha”, alisema.

 

Alisema tayari majaribio yamefanyika na yamekwenda vizuri na kupitia njia hiyo hata wanafunzi wa maeneo mbalimbali wanaokuwa wameunganishwa kwenye mfumo wanaonana. Pia alitaja mpango wa elimu kwa Njia ya mafunzo utakaowezesha wanafunzi kupata ujuzi na uzoefu. “Kwa hiyo wanafunzi wanaomaliza masomo yao katika vyuo mbali mbali, stashahada, na astashahada maana yake anakwenda kuanza ajira ya serikali kutakuwa na mafunzo ya vitendo kwa hiyo kutakuwa na mamilioni ya walimu,” alisema.

Leave A Reply

Your email address will not be published.